Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kunyimwa matibabu kwa mabaharia wa meli zilizotia nanga Afrika Magharibi si sahihi: Ripoti

Dawa za kukabiliana na Ebola.Picha ya WHO/M. Missioneiro

Kunyimwa matibabu kwa mabaharia wa meli zilizotia nanga Afrika Magharibi si sahihi: Ripoti

Umoja wa Mataifa na mashirika makubwa ya usafirishaji, biashara na utalii yameeleza wasiwasi wake juu ya ripoti za kunyimwa huduma ya afya mabaharia waliougua baada ya meli zao kutia nanga kwenye nchi zenye mlipuko wa Ebola.

Ripoti ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaoshughulikia dharura ya Ebola, UNMEER imekariri kikosi kasi kinachohusika na safari na usafirishaji kikitaka serikali kuzingatia mapendekezo ya shirika la Afya duniani WHO kuhusu masuala ya usafirishaji.

Mapendekezo hayo pamoja na mambo mengine yanazuia vitendo kama hivyo kwani hadi sasa hakuna zuio lolote la safari au biashara kwa nchi zilizokumbwa na Ebola.

Wakati huo huo, Senegal imetangaza kuwa itafungua mpaka wake na Guinea na kurejesha safari za anga baina yake na Liberia na Sierra Leone.

Ripoti ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kushughulikia dharura ya Ebola, UNMEER, imesema Rais Macky Sally wa Senegal amefikia uamuzi huo kufuatia mapendekezo ya jumuiya ya uchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS ya kutaka mipaka na nchi zilizokumbwa na Ebola ifunguliwe.

Hata hivyo Rais Sally hakutaja tarehe rasmi ya kufungua mpaka huo na Guinea au kuanza tena safari hizo za ndege.