Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OCHA yatenga dola milioni 8 kwa ajili ya Niger

Mkuu wa OCHA, Bi. Valerie Amos (Picha ya UM)

OCHA yatenga dola milioni 8 kwa ajili ya Niger

Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, Bi. Valerie Amos, ametenga zaidi ya dola millioni saba kwa ajili ya misaada ya dharura ya kibinadamu nchini  Niger.  Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Taarifa ya OCHA imesema fedha hizo ni ishara kuwa jumuiya ya kimataifa inaunga mkono  juhudi za serikali ya Niger za kushughulikia mahitaji ya kibinadamu kwa ushirikiano wa karibu na washirika.

Imesema fedha hizo zitasaidia kuendelea na utoaji wa misaada ya kibinadamu na kupunguza makali ya maisha kwa wananchi walio na mahitaji.

Niger kama nchi zingine zilizo Ukanda wa Sahel, inakabiliwa na uhaba wa chakula na aghalabu watoto 880,000 walio na umri wa chini ya miaka mitano wako hatarini kupata utapiamlo.