Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya kibindamu Iraq ya zidi kuzorota: Mratibu

Kevin Kennedy, Naibu Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq. (Picha:Unifeed)

Hali ya kibindamu Iraq ya zidi kuzorota: Mratibu

Hali ya kibinadamu nchini Iraq inazidi kuzorota kutokana na ongezeko la ghasia nchini humo ambazo hazionyeshi dalili za kufikia ukomo.

Naibu Mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Iraq, Kevin Kennedy amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari kwa njia ya video kutoka Iraq.

Amesema awali wakimbizi walikuwa wakipatiwa hifadhi na wenyeji lakini sasa hivi hakuna pa kuwaweka na wengi wao wanasaka hifadhi kwenye shule huku wakiwa wanakumbwa na kiwewe.

(Sauti ya Kennedy)

“Watu walioko hapa walikuja kusaka hifadhi. Walikimbia makwao  wakiwa na nguo na  vifaa vyao vichache sana ambavyo waliweza kubeba. Wamekuja na hali mbaya wakiwa wamejawa na fikra baada ya kuona mambo ambayo hawakutaka kuona na wakiwa wameacha ndugu zao.”

Naibu Mratibu huyo amesema wanajitahidi kutoa usaidizi lakini kuna changamoto wanazo kabiliana nazo.

Amezitaja kuwa ni mosi maeneo mengine hayafiki kikamavile Anbar, pili, ukosefu wa makazi na msimu wa baridi kali unawadia na maisha ya wakimbizi wa ndani  yatakuwa magumu zaidi.

Kwa mujibu wa Kennedy, wakimbizi wa ndani 166,000 wanahitaji makazi.