Burundi yasema haiwezekani kupuuza MDGS na kuanza upya

27 Septemba 2014

Itakuwa ni vigumu kupuuza malengo ya maendeleo ya milenia (MDGS) na kuanza upya. Amesema makamu wa rais wa Burundi Prosper Bazombaza wakati akihutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa katika kikao chake jumamosi ya leo.

Malengo ya milenia yaliyowekwa na viongozi wa dunia mwaka 2000 ambapo pamoja na mengineyo yako kuondoa umasikini , elimu ya msingi kwa wote na usawa wa kijinsia, yanafikia ukomo wake mwaka2015.

Makamu huyo wa rasi wa Burundia mesema tangu mwaka 2000 hatua zimepigwa katika kuondoa umasikini, kupunguiza vifo vya watoto wachanga na vifo vitokanavyo na malaria .

(SAUTI BAZOMBAZA)

"Ijapokuwa nchi zote hazina uzoefu sawa kuhusiana na hatua hizi, ukweli unabakia kuwa Burundi inakubalina na wazo kuwa itakuwa ni makosa kuyatelekeza malengo ya maendeleo ya milenia na kuanza upya. Kinyume chake tunachopaswa kufanya ni kuendelea na mageuzi yetu ambayo yametuletea maendeleo makubwa."

 

Bwana Bazombaza amesema kuwa licha ya kwamba Burundi haitatimiza malengo yote, imefanya kile alichokiita hatua zisizofaa kupuuzwa katika elimu, na afya. Amesema hili limefanyika kwa kutoa elimu bure, tiba kwa watoto walioko chini ya miaka mitano na akina mama waliojifungua.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter