Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ashutumu shambulio dhidi ya askari wa UNDOF

Walinda amani wa UNDOF wakiwa kazini. (Picha:UM-Maktaba)

Ban ashutumu shambulio dhidi ya askari wa UNDOF

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin Moon ameshutumu vikali shambulio la jumamosi dhidi ya vikosi vya Umoja wa Mataifa vya uangalizi wa uwekaji chini silaha, UNDOF vilivyopo milima ya  Golan.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa pia imemkariri Ban akishutumu kuendelea kuwekwa kizuizini na kudhibitiwa kwa askari 84 walinda amani kutoka Fiji na Ufilipino walioko kwenye kikosi hicho unaofanywa vikundi vilivyojihami visivyo vya kiserikali ikiwemo Al Nusra Front.

Katibu Mkuu ametaka kuachiwa askari hao bila mashariti kwa walinda amani hao na kutaka pande zote kushirikiana na UNDOF kuwezesha kikosi hicho kufanya kazi kwa uhuru na kuhakikisha usalama wa watendaji wake na mali zao.