Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya waliouawa Kabul yaongezeka, wafanyakazi wa UM waliouawa wafahamika

Idadi ya waliouawa Kabul yaongezeka, wafanyakazi wa UM waliouawa wafahamika

Idadi ya watu waliokufa kwenye shambulio la Ijumaa huko Kabul nchini Afghanistan, imeongezeka na kufikia 21 huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon akisema kuwa ni wakati mwingine wa majonzi kwa Umoja huo kwani wafanyakazi wake wanne wameuawa kwenye tukio hilo.

Amewataja wafanyakazi hao kuw ani Basra Hassan kutoka Marekani, Nasrin Jamal wa Pakistan, Kahnjar Wabel Abdallah wa Lebanon na Vadim Nazarov kutoka Urusi.

“Huu ni wakati mwingine wa majonzi kwa Umoja wa Mataifa ambapo wafanyakazi wenzetu wanne wameuawa kwenye shambulio la kigaidi huko Kabul. Natuma rambirambi kwa familia na nawatakia ahueni ya haraka majeruhi. Wakati Umoja wa Mataifa unahuzuni kutokana na tukio hilo na wahanga wake, tunaendelea kujizatiti kufanya kazi ya kuleta amani, utulivu na maendeleo nchini Afghanistan.”