Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tume huru ta UM kuhusu hali nchini Syria yatoa taarifa yake.

Tume huru ta UM kuhusu hali nchini Syria yatoa taarifa yake.

Tume huru ya kimataifa inayoendesha uchunguzi kuhusu Syria imesema kuwa taifa hilo linaendelea kuzama kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.  Akihutubia kikao cha Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Uswisi, Mwenyekiti wa tume hiyo Paulo Sérgio Pinheiro amesema sababu kuu ya kuwepo vifo vingi , kuhama kwa watu na uharibifu mkubwa nchini Syria ni vile ambavyo pande husika kwenye mzozo zinavyoendesha mikakati yao. Maoni yaliyokusanywa kutoka kwa watu 191 mwezi Februari yanaonyesha kuzorota kwa hali na kusambaa kwa ghasia kote nchini Syria huku kupungua kwa maeneo yaliyo salama yakichangia kwahama zaidi kwa watu. Taarifa hiyo inaeleza bayana mauaji ya halaiki yanayondelea nchini Syria kama anavyofafanua zaidi Bwana Pinheiro.

(SAUTI YA PINHEIRO)