Saudi Arabia yasaidia harakati za UM za kukabiliana na ugaidi; Ban ashukuru

13 Agosti 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameishukuru serikali ya Saudi Arabia kwa msaada wake wa dola Milioni Mia Moja kwa ajili ya kituo cha udhibiti wa ugaidi cha umoja huo, UNCCT.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutolewa kwa msaada huo Ban amesema kituo hicho ni kimetokana na ubunifu wa Saudia Arabia mwaka 2005 na wakati wa uzinduzi mwaka 2011 nchi hiyo ilitoa mchango wa dola Milioni 10.

Ban amesema mchango umekuja wakati muafaka kwani..

(Sauti ya Ban)

"Ongezeko la hivi karibuni la vitendo vya ugaidi kwenye nchi kadhaa na maeneo ya dunia, hasa vile vinavyoonyeshwa na kundi linalotaka kuunda serikali ya kiislamu nchini Iraq, ISIL, ni ishara ya changamoto zinazotukabili. Natarajia kituo hiki kuwa na dhima muhimu kwenye vitengo vyote 34 vya kikosi kazi vya Idara ya masuala ya siasa ili kuchagiza harakati za Umoja wa Mataifa dhidi ya ugaidi duniani.”

Kituo hicho kiko ndani ya kikosi kazi dhidi ya ugaidi CTITF cha Idara ya masuala ya siasa ya Umoja wa Mataifa.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud