Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raquelina ataja atakachofanya kwanza akiwa Katibu Mkuu wa UM

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon akiwa na Raquelina Langa. (Picha:UN /Mark Garten)

Raquelina ataja atakachofanya kwanza akiwa Katibu Mkuu wa UM

Mwanafunzi wa darasa la Kumi kutoka Msumbiji ambaye alialikwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kujionea shughuli za Umoja huo na kushiriki mkutano wa vijana amezungumzia hisia zake na vile ambavyo amejifunza katika kipindi hicho. Taarifa kamili na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Raquelina Langa ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa kuwa amejifunza mengi ikiwemo kujieleza na kubadilishana taarifa na wengine juu ya uzoefu wake huku akisema amekuwa anashangaa kwanini hakuna Katibu Mkuu mwanamke. Ndipo akaulizwa akipata wadhifa huo atafanya nini?

“Kwanza magonjwa, afya ya akili, mfano suala la vita na mizozo, baadhi ya nchi ambazo zinakuwa tegemezi halafu zinakumbwa na mizozo ya wenyewe kwa wenyewe kama nchi yangu. kwa hiyo kushughulikia masuala haya yote.”

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon akaeleza maoni yake kuhusu Raquelina..

“Unaweza kuwa na ndoto nzuri na matarajio mengi, lakini jaribu kusimamia dira yako na jitahidi ufikie lengo hilo.”