Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asikitishwa na kurejea kwa mapigano Gaza

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq Picha@UM

Ban asikitishwa na kurejea kwa mapigano Gaza

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameelezea masikitiko yake baada ya pande kewnye mzozo wa Gaza kushindwa kukubaliana juu ya kuongeza muda wa sitisho la mapigano lililomalizika jana.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan  Haq amesema Ban ameshutumu kuanza tena kwa urushwaji wa maroketi kuelekea Israel akisema machungu na vifo vinavyokumba raia walionasa kwenye mapigano haya vumiliki.

Ametaka pande hizo kutafuta haraka mbinu ya kurejesha makubaliano ya kusitisha mapigano kwa misingi ya kibinadamu na kuendelea mashauriano huko Cairo, Misri ili kufikia makubaliano ya dhati.

(Sauti ya Ban)

Katibu Mkuu anatoa wito wa dhati kwa pande zote kuacha kutumia njia ya kijeshi kwani hiyo itazidi kuzorotesha hali ya kibinadamu ambayo tayari imekumba Gaza.”

Ban amesema kuongezwa muda kwa sitisho la mapigano ni muhimu kwa mazungumzo kuweza kuendelea na kushughulikia masuala ya msingi ya mzozo huo haraka iwezekanavyo.