Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO na viongozi wa Afrika magharibi wajadili mpango wa kudhibiti Ebola

WHO/T. Jasarevic
Photo: WHO/T. Jasarevic

WHO na viongozi wa Afrika magharibi wajadili mpango wa kudhibiti Ebola

Wakati ugonjwa wa Ebola ukiendelea kuenea na kusababisha vifo huko Afrika Magharibi, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya duniani, WHO wanafanya mkutano huko Guinea-Conakry kuzindua mpango wa haraka kudhibiti ugojwa huo uliosababisha vifo vya watu 729 hadi sasa kati ya zaidi ya visa 1300 vilivyoripotiwa. Assumpta Massoi na taarifa kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Mpango huo mpya wa pamoja wa dola Milioni 100 ni sehemu ya kampeni za kimataifa, kikanda na kitaifa za kudhibiti Ebola inayoendelea kukumba Liberia, Guinea na Sierra Leone tangu mwei Machi mwaka huu huku nchi jirani zikiwa na hofu ya kupata maambukizi.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Margaret Chan amesema hofu hiyo inahitaji juhudi mpya ikiwemo kuongeza rasilimali fedha na watendaji kwani tayari nchi zilizokumbwa zimeainisha mahitaji yao na WHO sasa inatafuta usaidizi wa kimataifa kusongesha utekelezaji wa mpango huo.

Mahitaji kwa mujibu wa mpango huo ni mamia ya wahudumu wa afya kwenye maeneo yenye maambukizi ili kutoa tiba na kuzuia maambukizi mapya na kuongeza mfumo wa utambuzi wa ugonjwa kwa nchi jirani.

Domingos Simões Pereira ni waziri Mkuu wa Guinea-Bissau.

(Sauti Domingos)

"Tunafahamu kwamba pwani ya Afrika Magharibi inakabiliwa na Ebola, kwa hivyo sisi tunachukua hatua za kuzuia kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huu, na kuhakikisha kwamba ugonjwa huu ukiibuka hapa GUINEA BISSAU, tutakuwa na uwezo wa kutoa huduma hiyo ipasavyo."