Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali inaendelea kusambaratika Ukanda wa Gaza- Ripoti ya UNRWA

Picha@UNRWA

Hali inaendelea kusambaratika Ukanda wa Gaza- Ripoti ya UNRWA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwasaidia wakimbizi wa Palestina, UNRWA kupitia msemaji wake Chris Gunness, limetoa ripoti mpya kuhusu  hali kwenye ukanda wa Gaza kufikia sasa.

UNRWA imesema kuwa, kwa saa 24 zilizopita, idadi ya watu waliokimbia na kutafuta hifadhi ndani ya kituo cha UNRWA mjini Gaza imeongezeka maradufu toka 22,000 na kufikia zaidi ya watu 47,000. UNRWA inatumia majengo yake kuhifadhi wakimbizi  na sasa majengo 43 ikiwemo shule zinatumika kama makaazi katika ukanda wa Gaza.

Halikadhalika, idadi kamili ya wakimbizi haijulikani  kwani baadhi ya wakimbizi wametafuta hifadhi kwa jamii na marafiki zao.

UNRWA imeomba ufadhili wa zaidi ya Dola Milioni 60 ili kukabiliana na  hali hiyo.

UNRWA imetoa wito kwa pande zote katika mzozo kuheshimu sheria ya kimataifa ya kibinadamu ya kulinda raia , wafanyi kazi wa huduma za kibinadamu na pia kulinda hadhi ya majen