Ufadhili zaidi unahitajika kuwahudumia wakimbizi waSudan Kusini walioko Uganda:WFP

17 Julai 2014

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limepaza sauti likiomba msaada zaidi ili liweze kushughulikia wakimbizi wanaoendelea kumiminika Kaskazini mwa Uganda kutoka Sudan Kusini.

Taarifa kamili na John Kibego wa Redio washirika ya Spice FM, nchini  Uganda.

 (Tarifa ya Johhn Kibego)

 Shirika la WFP linaomba kupigwa jeki zaidi wakati ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR)likisema, linaendelea kupokea kati ya wakimbizi 100-150 kutoka Sudan Kusini kila siku.

Ombihilolimetolewa na Alice Martin-Daihirou, Mwakilishi wa WPF nchini humo wakati akiongea na Balozi wa Ufaransa nchini Uganda Sophie Makame mjiniKampala.

Aidha, Daihirou aliishukuru serikali ya Ufaransa kwa kutoa msaada wa chakula kinachogharimu US$ 272,000 tangu mgogoro wa kisiasa uzuke Sudan Kusini Disemba mwaka Jana.

Balozi Sophie ambaye alitembelea ghala la chakula la WFP mjiniKampalasiku ya Ijumaa alisema, Ufaransa itajitoa kadri iwezavyo kusaidia kushughulikia wakimbizi wanaoendelea kumiminika nchini humo.

Shirika la Chakula Duniani (WFP) lililazimika kukata mgao wa chakula kwa baadhi ya wakimbizi kwa asilimia 50% wakati mapigano yalikuwa yameshamiri Sudani Kusini Disemba mwaka jana.

WFP itaendelea kutoa mgao wa 100% baada ya kipigwa jeki ya US$ 10 m. na serikali ya Marekani.

Kwa mujibu wa UNHCR, kuna takriban wakimbizi 120,000 wa Sudan Kusini ambao wameingia nchiniUgandatangu mapigano yazuke nchini mwao mwezi Disemba mwaka uliyopita.