Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maendeleo Afrika yamulikwa kwenye Baraza Kuu

Kikao cha Baraza Kuu Picha/UM

Maendeleo Afrika yamulikwa kwenye Baraza Kuu

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo limefanya mdahalo kuhusu kuendeleza kwa uwekezaji barani Afrika na mchango wake katika kufikia malengo ya maendeleo ya bara la Afrika, yakiwemo kutokomeza umaskini na kufikia ukuaji na maendeleo endelevu na jumuishi ya kiuchumi.

Akizungumza wakati wa mdhahalo huo, rais wa Baraza Kuu John W. Ashe, amesema kuwa katika mwongo mmoja uliopita, kumekuwa na uwekezaji mkubwa katika nchi nyingi barani Afrika, lakini uwekezaji huo umehusu utegaji wa rasilmali na kuziuza, bila kuongeza uzalishaji na kubuni nafasi za ajira.

(SAUTI YA ASHE)

Licha ya kuwepo utajiri mkubwa wa maliasili, hakujakuwa na usambazaji faida zake na mapato yatokanayo na mavuno ya maliasili hizo, au kuzitumia kukuza viwanda na mikakati ya maendeleo. Kwa sababu hii, bado kuna kasoro za ufadhili, hususan katika kilimo, usindikaji na maendeleo ya miundo mbinu. Kuwekeza katika kilimo kutatoa matumaini kwa bara Afrika.”

Katibu Mkuu Ban Ki-moon pia amezungumza, akitaja vitu vitatu vinavyohitajika ili kumaliza umaskini uliokithiri na kuendeleza maendeleo jumuishi barani Afrika

Kwanza, mazingira yanayowezesha na kuchagiza uwekezaji na kupunguza hatari, pili, uwekezaji unaofaa. Tatu, udhibiti wa busara wa mapato ili yasaidie maendeleo endelevu.”