Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya idadi ya watu yamulika vijana milioni 1.8 waliopo duniani

UNFPA/Idriss Qarqouri (NICA ID:587729)

Siku ya idadi ya watu yamulika vijana milioni 1.8 waliopo duniani

Leo tarehe 11 Julai ikiwa ni siku ya idadi ya watu duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amewaomba viongozi wote duniani kuwekeza katika hatma ya vijana, akisema vijana milioni 1.8 waliopo duniani, hasa katika nchi zinazoendelea, wana nguvu za kupambana na changamoto zinazokumba ulimwengu, lakini bado wananyimwa fursa ya kupta elimu bora, kazi imara na nafasi ya kushiriki kwenye jukwaa la kisiasa. Taarifa kamili na Amina Hassan

(Taarifa ya Amina Hassan)

Ban ametiwa wasiwasi zaidi kuhusu hali ya wasichana wanaokabiliana na ubaguzi, ukatili wa kijinsia, ndoa na mimba za utotoni.

Hata hivyo, amesema kuwa amefurahi kuona kwamba vijana wanashirikiana na wanapaza sauti zao, wakiomba wapewe kipaumbele katika ajenda ya maendeleo. Ameongeza kuwa kuwawezesha vijana kutajenga mustakhabali endelevu kwa vizazi vijavyo.

Halikadhalika, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu, UNFPA, Babatunde Osotimehin, amesema, anaamini vijana wa siku hizi wanaelewa zaidi haki zao na matarajio yao, kwa hiyo, wakipatiwa elimu, afya, na nafasi ya kujumuishwa kisiasa, wanaweza kutokomeza umaskini unaoendelea duniani.