Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF, EU na Libya zabuni mfumo wa udhibiti wa takwimu za Elimu

Watoto wakiingia shule iliyomo ndani ya tenti la UNICEF katika kambi la Shousha mpakani mwa Libya na Tunisia. UNICEF/Heifel Ben Youssef.(UN News Centre)

UNICEF, EU na Libya zabuni mfumo wa udhibiti wa takwimu za Elimu

Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF, kwa ufadhili kutoka Muungano wanchi za Ulaya, EU, limeisaidia Wizara ya Elimu nchini Libya kubuni mfumo wa udhibiti wa takwimu za elimu, EMIS, ambao utaiwezesha Libya kuwa na uhakika kuhusu jinsi mfumo wake wa elimu ulivyo.

Mfumo wa EMIS utatumiwa kama chombo stahiki cha kufuatilia ikiwa mfumo wa elimu katika shule za malezi, msingi na sekondari unatimiza malengo yake, na utaimarisha ukusanyaji wa maelezo na takwimu, kufanya tathmini, matumizi na usambazaji wa takwimu hizo.

Mfumo huo pia utawawezesha wasimamizi na watunga sera wa elimu kufanya maamuzi yanayotokana na takwimu na maelezo ya kutegemewa, ili kuboresha mfumo mzima wa elimu nchini Libya, ili uwanufaishe watoto na familia zote.