Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Mazingira latamatishwa na matumaini

Baraza la Mazingira latamatishwa na matumaini

Mkutano wa kwanza wa Baraza la Mazingira duniani  umefanyika wiki hii huko Nairobi Kenya, maudhui ya jumla yakiwa ni malengo ya maendeleo endelevu na ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015. Huo ulikuwa ni mkutano wa kwanza wa chombo hicho kilichoundwa kufuatia mkutano wa Rio +20 nchini Brazili mwezi Juni mwaka 2012 wa kutaka kuanzishwa kwa mamlaka simamizi ya shirika la mazinigira duniani, UNEP. Mada zililenga mambo mbali mbali ikiwemo kudhibiti ujangili na biashara haramu ya viumbe na mazao ya porini, uchangiaji shughuli za kiuchumi zinazojali mazingira na kuondoka na uchafuzi wa mazingira. Je ni yapi yaliyoafikiwa? Basi ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.

Wimbo…

 Ni karibishohilokwa wajumbe wa mkutano wa Baraza la mazingira uliotamatishwa Ijumaa mjiniNairobiKenya. Mkutano umefanyika kukiwa na wimbi kubwa la ujangili wa wanyamapori hususan Tembo na Faru na eneo la Afrika Mashariki, kitendo kilichohusishwa na ukosefu wa usalama.

Mathalani ripoti ya shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP na lile la kimataifa la polisi iliyotolewa wakati wa mkutano ilioanisha ujangili na uhalifu ikisema kikundi kimoja cha kigaidi kinachoendesha shughuli zake Afrika Mashariki chakadiriwa kupata kati ya dola Milioni 38 na Milioni 56 kila mwaka kutokana na biashara haramu ya mkaa. Hili likatoa mwamko kwa wana Afrika Mashariki kwani kidole kimoja hakivunji chawa! Lazaro Nyalandu, Waziri wa Maliasili na UtaliiTanzania.

(Sauti ya Nyalandu)

 Pamoja na juhudi za kikanda,Tanzanianayo ikaelezea hatua za kitaifa.

(Sauti ya Nyalandu-2)

Suala la sheria na mazingira nalo lilimulikwa na ndio msingi wa kuwajumuisha majaji na mahakimu kwenye mkutano  huokamaanavyosema Elizabeth Mruma-Mrema, Naibu Mkurugenzi Idara ya sera za mazingira na utekelezaji, DEPI ndani ya UNEP.

(Sauti ya Elizabeth)

Bi Mrema akasema sheria hafifu na dhaifu huzaa hukumu hafifu na zisizojali mazingira akirejea hali ilivyokuwa zamani..

(Sauti ya Elizabeth)

Pamoja na mawaziri, majaji na mahakimu, walikuwepo pia washiriki kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali yenye ajenda sawa na UNEA. Miongoni mwao ni asasi ya Alive and Kicking iliyoanzishwa hukoKenyamwaka 2004. Asasi huu hushona mipira ya soka na kuiuza ikiwa na ujumbe wa afyakamavile Malaria na Ukimwi. Lakini sasa liko na ushirikiano na UNEP na mwakilishi wake Rose Maketi anasema pamoja na kuwapatia ajira vijana na watu wazima, wanalinda pia mazingira na wanyamapori.

(Sauti ya Rose)

Huku wakishona mipira na kuhifadhi mazingira, Alive and Kicking inaboresha pia maisha ya washona mipira hiyo,

(VOXPOPS)

Akikunja jamvi la mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema ujumbe uko dhahiri ya kwamba kulinda mfumo wa usaidizi wa uhai wa binadamu ni muhimu kwa maendeleo endelevu na ni  jukumu la kila mtu, na zaidi ya yote..

(Sauti ya Ban)

“Nashukuru kazi yenu ya miaka yote hii lakini huu ni mwanzo! Mabadiliko ya dhahiri! Suluhu zipo! Kasi inasonga na huu ni wakati wa kuongoza!”