Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia mpya CAR zafurumusha wengi kutoka makwao:UNHCR

Melissa Flemming, msemaji wa UNHCR Geneva. (Picha@UM/Maktaba)

Ghasia mpya CAR zafurumusha wengi kutoka makwao:UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema lina hofu juu ya ghasia mpya zilizoibuka wiki hii huko Jamhuri ya Afrika ya Kati kwenye mji wa Bambari ambapo watu wapatao 45 wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa.

Ghasia hizo zilianza jumatatu baada ya watu wenye silaha kushambulia kambi moja Kusini mwa mji wa Bambari inayohifadhi waislamu kutoka kabila la Peul, jambo lililosababisha kulipiziana visasi mjini humo baina ya raia. UNHCR inasema mji huo ulio kilometa 380 kaskazini-mashariki mwaBangui, sasa umebakia gofu

Melissa Flemming ni msemaji wa UNHCR, Geneva na anasema kinachoendelea kinakwamisha operesheni zao.

(Sauti ya Melissa)

Fukuto la ghasia limekuwepo huko Bambari tangu mwezi Mei baada ya mapigano kusababisha watu zaidi ya 13,000 kupoteza makaziyao.