Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazao mbadala pekee si suluhu ya kutokomeza madawa ya kulevya:Ashe

John William Ashe, Rais wa Baraza kuu la UM.@UNPhoto/Evan Schneider

Mazao mbadala pekee si suluhu ya kutokomeza madawa ya kulevya:Ashe

Katika siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya madawa ya kulevya na usafirishaji haramu wa bidhaa ikiwemo madawa ya kulevya, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa John Ashe ametaka serikali kuendelea kuwapatia wananchi wake fursa mbadala za kujikwamua kiuchumi ili kuondokana na tatizo la madawa ya kulevya.

Ashe amesema ingawa serikali zimeanza kutekeleza misingi ya ongozi ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu njia mbadala za maendeleo kwa wakulima wa mazao yatumikayo kutengeneza madawa ya kulevya, hatua zaidi zinahitajika.

Amesema wakulima wakipatiwa mazao mbadala ya kilimo, wanahitaji miundombinu sahihi ili kuweza kufikisha mazao hayo sokoni, na zaidi ya yote uhakika wa masoko ya bidhaa hizo.

Bwana Ashe ametaka mtazamo mpana zaidi wa usaidizi huo wa njia mbadala kwani madawa ya kulevya siyo tu yanakwamisha kufikia maendeleo endelevu bali pia yanakwamisha juhudi za kutokomeza umaskini na kuondoa tofauti za usawa.