Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya mazingira duniani, wakazi songea nchini Tanzania wapanda miti bonde la Songambele:

Upandaji miti sahihi kwenye eneo husika hulinda mazingira halisi ya eneo hilo.@UNEP

Siku ya mazingira duniani, wakazi songea nchini Tanzania wapanda miti bonde la Songambele:

Tarehe Tano Juni kila mwaka ni siku ya mazingira duniani ambapo ni fursa ya kutathimini hatua za kulinda mazingira kwani dunia inakabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi. Athari hizo zinasababisha mabonde ya maji kukauka, joto kuongezeka na hata wakazi kushindwa kuendelea na shughuli zao za kila siku za kujipatia kipato. Huko RuvumaTanzaniahii leo wakazi wa mjini Songea eneo la Bombambili wamechukua hatua kwa kupanda miti kwenye bonde la Songambele. Je wamepanda miti gani na nini kilichowasukuma wao binafsi? Basi ungana na Tamimu Adamu wa Radio washirika Jogoo FM hukoRuvumakatika makala hii.