Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujasiriamali ni lulu kwa wanawake Afghanistan

Gul Shrin, mwanamake mjasiriramali Afghanistan. Picha: UM/Video capture

Ujasiriamali ni lulu kwa wanawake Afghanistan

Wanawake nchini Afghanistan wamekuwa mfano kwenye jamii zao katika utekelezaji wa usemi “penye nia pana njia”. Hii ni baada ya kukujikita katika masuala ya ujasiriamali ili kujikwamua na umasikini. Wanajihusisha na shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo cha mboga mboga na ufundi cherehani. Na kipato wanachokipata kinawafaa wao, familia zao na jamii kwa ujumla. Ungana na Patrick Newman katika Makala hii ikitukutanisha na kina mama hao.