Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano kuhusu mabadiliko ya tabianchi kuanza Bonn, Ujerumani

Mkutano kuhusu mabadiliko ya tabianchi kuanza Bonn, Ujerumani

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Awamu nyingine ya midahalo kuhusu mabadiliko ya tabianchi itaanza mjini Bonn, Ujerumani, mnamo Juni 4, ikiwaleta pamoja mawaziri ambao wanatarajiwa kujadili masuala muhimu ya kisiasa ambayo yanaweza kupatiwa suluhu, kama maandalizi ya mkataba kuhusu mabadiliko ya tabianchi, ambao unatarajiwa mjini Paris, mwaka 2015.

Wawakilishi wa serikali wataendelea na shughuli zao za kubuni mkataba mpya wa 2015, na kutafuta njia za kuongeza kasi ya sasa ya kimataifa ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kabla ya mwaka 2020, wakati mkataba huo unatarajiwa kuanza kutekelezwa.

Katibu Mtendaji wa wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, UNFCCC, Christiana Figueres, amesema kote duniani, nchi nyingi, wafanyabiashara, miji, wawekezaji na watu wengineo wanachukua hatua kuhusu mabadiliko ya tabianchi, na kwamba serikali sasa zinashughulikia michango yao ya kitaifa ili kufikia mkataba mpya mnamo mwaka 2015.