Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuongeze kasi katika juhudi za kukabiliana na vifo vya watoto na waja wazito: Ban

UN Photo/Eskinder Debebe)
Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon akihutubia mkutano huo. (Picha:

Tuongeze kasi katika juhudi za kukabiliana na vifo vya watoto na waja wazito: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ametoa wito kasi iongezwe katika juhudi za kuendeleza hatua za kukabiliana na vifo vya utotoni na waja wazito. Taarifa kamili na Assumpta Massoi.

Bwana Ban ametoa wito huo wakati wa mkutano wa kimataifa wa kuunga mkono mkakati wa Kila Mwanamke, Kila Mtoto, ambao unafanyika mjini Toronto, Canada. Kwenye mkutano huo ambao pia umehudhuriwa na Rais Jakaya Kiwete wa Tanzania, Katibu Mkuu ametolea mfano wa familia yake mwenyewe, ambapo ndugu zake wa kwanza wawili walifariki utotoni.

Bwana Ban amesema wanawake wengi, hususan katika nchi zinazoendelea kama barani Afrika na Kusini Mashariki mwa Asia, hazina huduma za afya ya uzazi kwa wote, na bado waja wazito wengi wanategemea tu akina mama wazee kama wakunga kutokana na uzoefu wao.

Katibu Mkuu amesema ingawa vifo vya waja wazito vimepunguzwa kwa takriban asilimia 50 tangu 1990 na vifo vya watoto kupunguzwa kwa kiasi kikubwa, bado juhudi zaidi zinahitajika, ili kuongeza kasi ya kuendeleza mwenendo huu