Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS yakutana na DAVID YAU YAU kujadili amani

UNMISS yakutana na DAVID YAU YAU kujadili amani

Mwakilishi maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini, Hilde Johnson amekutana na kuwa na mazungumzo na kiongozi wa kikundi kinzani cha SSDM/A David Yau Yau ambapo amekaribisha kutiwa saini kwa makubaliano ya amani kati ya kikundi hicho na serikali mapema mwezi huu.

Bi. Johnson ambaye ni mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, UNMIS amesifu dhima ya Yau Yau katika kuwezesha suluhu la mzozo kwenye mji wa Greater Pibor County, jimbo la Jonglei huku akirejelea utayari wa UNMISS wa kusaidia utekelezaji kamilifu wa hatua hiyo ambayo amesema ni msingi wa amani ya kudumu kwa wakazi wa Pibor na jirani zao.

Kwa upande wake Yau Yau amesisitiza uharaka wa kutekeleza makubaliano hayo na kuwapati wakazi wa Greater Pibor manufaa ya uwepo wa amani na utulivu miongoni mwa jamii zilizoathirika.

Mwakilishi huyo maalum amesema ni matumaini yake kuwa serikali ya Sudan Kusini na wapinzani watafuata mkondo huo na kumaliza mzozo unaoendelea kusababisha machungu kwa wananchi wa Sudan Kusini.