Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhifadhi wa mazingira Rwanda, wainua utalii na fursa mpya za ukuaji: UNEP

Uhifadhi wa mazingira (Picha:UN Poverty and Environment Initiative )

Uhifadhi wa mazingira Rwanda, wainua utalii na fursa mpya za ukuaji: UNEP

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP limezungumzia hatua zilizochukuliwa na Rwanda katika kuhifadhi mazingira kama njia mojawapo ya kuinua kiwango cha utalii na ukuaji wa uchumi.

Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya UNEP inataja hatua zilizochukuliwa na Rwanda kuwa ni pamoja na uhifadhi wa sokwe wa milimani na maeneo oevu kwenye maeneo ya Nyabarongo-Akagera na Rugezi, hatua ambazo sasa zinazaa matunda.

Sokwe aina ya kipekee beringei graueri walio hatarini kutoweka hupatikana zaidi kwenye mbuga ya Viruka iliyoko ukanda huo wa maziwa makuu ambapo Rwanda kwa kushirikiana na Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamekubaliana kuhifadhi mazingira ya eneo hilo ili kuwalinda sokwe hao.

Takwimu zinaonyesha hatua hizo kuwezesha idadi ya watalii kuongezeka kutoka 1200 mwaka 2000 hadi 7417 mwaka 2004, huku biashara za vikapu vinavyotengenezwa na wakazi wa maeneo hayo nayo kupanuka kwani bei ya kikapu imepanda kutoka dola Mbili hadi 10.