Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa heshima wa IOC ateuliwa kuwa mjumbe wa Ban kwa wakimbizi vijana na michezo

Rais wa heshima wa IOC ateuliwa kuwa mjumbe wa Ban kwa wakimbizi vijana na michezo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametangaza kumteua Dkt. Jacques Rogge wa Ubelgiji kuwa mjumbe wake maalum wa masuala ya wakimbizi vijana na michezo.

Akitambuliwa kwa mchango wake katika kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Mataifa kupitia malengo ya milenia na ajenda ya 21 ya mazingira, Dkt. Rogge atasaidia kuendeleza matumizi ya michezo kwa ajili ya kuinua vijana wakimbizi ili kuelekea kwenye amani, maridhiano, usalama, afya, usawa wa kijinsia na jamii shirikishi.

Wakati akiwa Rais wa IOC kati ya mwaka 2001 hadi 2013 Dkt Rogge alikuwa kichochea cha kuendeleza maadili ya olimpiki hususan katika nyanja za elimu, utamaduni, maendeleo ya wanawake na mazingira.

Yakadiriwa kuwa zaidi ya watu Milioni 44 duniani ni wakimbizi na waathirika zaidini vijana na watoto.