Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Filamu zaendelea kuleta msisimko lakini wabunifu mashakani:WIPO

Filamu zaendelea kuleta msisimko lakini wabunifu mashakani:WIPO

Ulimwengu unaadhimisha siku ya hakimiliki duniani tarehe 26 Aprili, maudhui ni Filamu: Msisimko wa dunia! Shirika la hakimiliki duniani, WIPO linasema filamu miaka nenda miaka rudi zimesaidia jamii kujifunza mambo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa na hata wakati mwingine kuwafikisha watazamaji maeneo ambayo hawajafika. WIPO inatoa pongezi kwa wabunifu wa filamu hizo na washiriki lakini wakitoa angalizo kuwa mwelekeo wa uwepo wa kazi hizo uko mashakani kwani teknolojia pamoja na kusaidia kuboresha filamu, inawezesha kutazamwa bila malipo na kukiukwa suala la hakimiliki bunifu. Je hali ikoje barani Afrika? WIPO inapendekeza nini? Basi ungana na Priscilla Lecomote katika makala hii.