Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Malaria inazuilika tuwekeze na tuitokomeze: Rais Baraza Kuu

Malaria inazuilika tuwekeze na tuitokomeze: Rais Baraza Kuu

Leo ni siku ya Malaria duniani ambapo Umoja wa Mataifa unasema takribani nusu ya wakazi wa sayari hii wakohatarini kukumbwa na ugonjwa huo unaoua watu zaidi ya Laki Sita kila mwaka wengi wao ni watoto huko Afrika. Ripoti ya Alice Kariuki inafafanua zaidi.

(Taarifa ya Alice)

Ujumbe wa siku hii kutoka Rais wa Baraza Kuu John Ashe unataka jamii ya kimataifa kutambua kuwa kazi kubwa imefanyika kutokomeza ugonjwa lakini hakuna kupumzika kwani maeneo mengi bado yako hatarini.

Ashe anasema ijapokuwa vifo vya watoto kutokana na Malaria Afrika vimepungua kwa asilimia 54 tangu mwaka 2000 bado kila dakika kuna mtoto anafariki dunia hivyo kwa kuwa ugonjwa huo unazuilika ni vyema kuchukua hatua haraka na kuwekeza mbinu sahihi za kinga na tiba ili kuondoa mzigo wa Malaria..

Nchini Tanzania vifo vya Malaria vimepungua lakini mganga mfawidhi kutoka hospitali ya rufaa mkoani Ruvuma Benedicto Ngaiza anasema changamoto sasa ni kupata takwimu sahihi.

(SAUTI BENEDICTO-1)

Kadhalika mganga huyo mfawidhi anaeleza mikakati ya kupambana na malaria.

(SAUTI YA BENEDICTO-2)