Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tutumie fursa ya teknolojia kuboresha sanaa ya filamu badala ya kuzikwapua: WIPO

Tutumie fursa ya teknolojia kuboresha sanaa ya filamu badala ya kuzikwapua: WIPO

Sekta ya filamu ni mjumuiko wa hakimiliki bunifu ambazo zinapaswa kulindwa ili jamii iendelee kunufaika na kazi hiyo ya sanaa ambayo sasa imeenea duniani kote, amesema Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kimataifa la hakimiliki WIPO Francis Gurry katika ujumbe wa siku ya hakimiliki duniani tarehe 26 mwezi huu.

Amesema sekta ya filamu inazidi kuenea duniani kote na kusaidia ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii lakini kuna mkwamo kwani teknolojia inayotumika vibaya kurahisisha ukwapuaji wa kazi hizo adhimu. Hivyo akatoa ujumbe..

(Sauti ya Gurry)

“Utakapotizama filamu wakati mwingine fikiria wabunifu wote walioandaa filamu hiyo na kumbuka kuna hakimiliki inayowawezesha kupata kipato chao. Na pili fikiria changamoto ya digitali kwa kuwa nafikiri hii ni wajibu wa kila mtu siyo watunga sera pekee. Ni vipi tunaweza kutumia fursa hii ya kipekee ya intaneti ya kueneza utamaduni na wakati huo huo kuhakikisha wabunifu wanaendelea kubuni na wanapata kipato chao kwa kuandaa filamu zinazoboresha maisha uetu.”

Mmoja wa waigizaji mashuhuri nchini Tanzania Jacob Steven al maarufu JB ni shuhuda wa kile kinachowakumba.

(Sauti ya Jacob Steven)

Mahojiano kamili na Jacob Steven kuhusu mustakhbali wa sekta ya filamu Tanzania yatapatikana kwenye ukurasa wetu.