Ukatili wa kingono katika vita ni uhalifu uloenea duniani kote: Bangura

24 Aprili 2014

Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu kuhusu ukatili wa kingono katika maeneo ya vita, Zainab Hawa Bangura, amesema kuwa ukatili wa kingono katika vita ni uhalifu ambao umeenea katika maeneo yote duniani.

Bi Bangura amesema hayo katika mkutano na wandishi wa habari mjini New York, wakati akizindua ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu ukatili huo wa kingono, ambayo inabainisha hali katika kipindi cha mwaka mmoja, kuanzia Januari hadi Disemba 2013.

Ripoti hiyo inaangazia hali katika nchi 21 Ulaya, Asia, Afrika, Amerika ya Kusini na Mashariki ya Kati.

Bi Mangura amesema ripoti hiyo inabainisha hatua zilizopigwa na changamto sugu ambazo bado zipo katika kupiga vita jinamizi la ukatili wa kingono katika vita.

(Sauti ya Bangura)

Bi Bangura amesema ni lazima kuhakikisha kuwa wahalifu wanaotekeleza ukatili huu hawakwepi mkono wa sheria kwa mikataba ya amani na marekebisho ya sekta za usalama ambayo hayazingatii ukatili wa kingono.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud