Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tofauti zozote zinazoanza kujitokeza zishughulikiwe kuepusha mauaji:Balozi Mulamula

Tofauti zozote zinazoanza kujitokeza zishughulikiwe kuepusha mauaji:Balozi Mulamula

Miaka 20 baada ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda, bado Umoja wa Mataifa unasema kuna viashiria penginepo vya uwezekano wa kutokea mauaji ya aina hiyo ikizingatiwa yanayoendelea huko Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan Kusini. Je nini nchi zinapaswa kufanya? Balozi Liberata Mulamula, Katibu Mtendaji wa kwanza wa Mkutano wa kimataifa wa Maziwa Makuu, ICGLR amemweleza Assumpta Massoi wa Idhaa hii katika mahojiano maalum kuwa hatua zinapaswa kuchukuliwa pindi fukuto zinapoanza. Hapa anaanza kwa kuelezea dhima ya nchi jirani katika maridhiano Rwanda na kuepusha mauaji kwenye Ukanda wa Maziwa makuu.