Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Yatosha, sasa tuchukue hatua kulinda mwanamke na mtoto wa kike:UM

Yatosha, sasa tuchukue hatua kulinda mwanamke na mtoto wa kike:UM

Machi Nane ya kila mwaka, dunia huadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake ambapo lengo ni kumulika utekelezaji wa haki za wanawake kwa kuzingatia kuwa tayari kuna mkataba wa kimataifa wa kupinga vitendo vyovyote vya ubaguzi dhidi ya wanawake, CEDAW. Mwaka huu tochi inamulika zaidi vitendo vya ukatili, majumbani, makazini, sehemu za biashara, kwenye migogoro na hata sehemu za amani ambako bado fikra za watu zinaruhusu ukatili. Na ukatili unaweza kuwa hata ndo za lazima kwa watoto wadogo, wanawake kubakwa vitani, kunyimwa fursa za ajira na kadhalika. Basi ungana na Assumpta Massoi katika makala haya yanayoanzia hapa New York, Marekani hadi Burundi, barani Afrika.