Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo hakuna ripoti za mapigano Malakal:UNMISS

Leo hakuna ripoti za mapigano Malakal:UNMISS

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS umesema shambulio la jana lililofanywa na jeshi la serikali, SPLA dhidi ya vikundi vilivyojihami limewezesha utulivu kwenye mji wa Malakal ulioko jimbo la Upper Nile.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amenukuu ujumbe huo ukisema kuwa hali leo ni shwari na vikosi vya serikali vimejiimarisha mjini humo .

Amesema kundi kubwa la askari wa serikali lilionekana likielekea eneo la kaskazini mwa Malakal na kwamba jeshi hilo limejizatiti kulinda raia 21,500 waliokimbia makwao na kusaka hifadhi kwenye ofisi za UNMISS.