Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya nusu ya silaha za kemikali Syria imeondolewa au kuharibiwa:UM

Zaidi ya nusu ya silaha za kemikali Syria imeondolewa au kuharibiwa:UM

Jopo la pamoja la Umoja wa Mataifa na shirika la kimataifa la kupinga silaha za kemikali, OPCW lenye jukumu la kusimamia uteketezaji wa mpango wa silaha za kemikali nchini Syria limesema zaidi ya nusu ya silaha hizo zimeshaondoshwa au kuharibiwa.

Ripoti hizo ni kwa mujibu wa taarifa ya jopo hilo wakati huu inapozingatiwa kuwa azimio la Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, linataka silaha zote za kemikali Syria ziwe zimeteketezwa ifikapo mwishoni mwa Juni mwaka huu.

Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq akawaeleza waandishi wa habari kuwa taarifa hizo zinatia moyo.

(Sauti ya Farhan)

“Hii inawasilisha maendeleo muhimu. Jopo la pamoja linasifu kasi iliyofikiwa na inachagiza serikali ya Syria kuendeleza kasi hiyo.”

Shehena za silaha hizo za kemikali zinaondoshwa Syria kupitia bandari ya Lattakia na inajumuisha kemikali hatarishi zaidi.