FAO yataka usawa wa kijinsia kwenye sekta ya Kilimo

7 Machi 2014

Katika kuadhimisha siku ya wanawake Machi Nane mwaka huu, Shirika la Chakula na Kilimo duniani, FAO limeendesha tukio la ngazi ya juu hii leo huko Roma, Italia likiangazia usawa wa kijinsia kwenye kutokomeza njaa na kuimarisha mifumo endelevu ya chakula. Taarifa zaidi na Alice Kariuki.

(Taarifa ya Alice)

Tukiohilolilihusisha viongozi waandamizi wa Umoja wa Mataifa akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa FAO José Graziano da Silva maadhimisho ya mwaka huu yamekuja wakati muafaka wakati wa mwaka wa kimataifa wa kilimo cha kaya.

Amesema nguvu kazi kubwa kwenye kilimo hicho ni wanawake hivyo usawa wa kijinsia ni muhimu ili kutokomeza njaa.

(Sauti ya da Silva)

Washiriki wa mkutano huo wamejadili changamoto wanazopata wanawake vijijini wanaotumia zaidi kilimo cha kujikimu ili kutunza familia zao lakini mara nyingi hutwama katika lindi la umaskini kutokana an kushindwa kupata ardhi stahili, maji, mafunzo ya kilimo bora na hata pembejeokamavile mbolea na vifaa.