Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanwamitindo Naomi Campbell awataka wanawake kujitokeza kupinga ukatili wa kijinsia

Mwanwamitindo Naomi Campbell awataka wanawake kujitokeza kupinga ukatili wa kijinsia

Mwanamitindo maarufu Naomi Campbell amewataka wanawake kuwa na matumaini na kujitokeza kupinga ukatili dhidi ya wanawake.

Akiongea katika mahojiniano maalum na Leda Letra wa idhaa ya Umoja wa Mataifa ya Kireno muda mfupi kabla ya kushiriki matembezi ya wanawake ya kuhamisha kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, mwanamtindo huyo amesema licha ya kuwa harakati hizo zaweza kuacha makovu lakini jambo muhimu ni:

(SAUTI NAOMI)

Nadhani kuwa na matumaini, inaweza kuwa jambo la kuacha kovu la kudumu ndanI yetu wote , nafikiri wanAwake wengi hapa leo watakuwa werevu na kuweka hayo pembeni na kuwasadia wengine na kusimama kupinga ukatili dhidi ya wanwake.