Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bei za vyakula zaongezeka mwezi February : FAO

Bei za vyakula zaongezeka mwezi February : FAO

Hali mbaya ya hewa,kuongezeka kwa mahitaji pamoja na usalama ni miongoni mwa sababu za kupanda kwa bei ya chakula kwa mwezi February duniani hususani katika nchi ambazo ni kinara katika uzalishaji wa chakula limesema shirika la chakula nakilimo duniani FAO. Joseph Msami na taarifa kamili

(TAARIFA YA MSAMI)

Kwa mujibu wa FAO bei za vyakula zimepanda kwa asilimia 2.6 katika mwezi February kiwango ambacho ni kikubwa zaidi tangu katikati ya mwaka 2012.

Vyakula vilivyoongezeka zaidi ni pamoja na sukari, mafuta, na nafaka katika mwezi January huku ngano, na bei za nafaka zikitajwa kupanda kutokana na mvutano wa hivi karibun kati ya Ukaraine na Urusi. Nchi zenye migogoro zikiwamo Sudani Kusini, Syria, Yemen, na Jamhuri ya Afrika ya Kati zinaendelea kukabiliana na ukosefu wa chakula kutokana na hali za dharura.

Concepción Calpe ni mchumi mwandamizi wa FAO

(SAUTI CALPE)

Inategemea zaidi waagizaji, kiasi gani watakuwa nacho, bei zipi watakabiliana nazo wakati wa kununua na kwa wauzaji ni kiasi gani watapata wakati wa kuuza bidhaa. Kabla ya kushuhudia mabadiliko kwa upande wa cha wauzaji wa rejareja na jumla itachukua muda. Huwezi kuona moja kwa moja bei za kimataifa zikiongezeka na kuona haraka madhara katika masoko ya ndani, itakawia. Kwa sababu mwaka 2013 mazao yalikuwa mazuri sana kwa ujumla, hifadhi ya chakula ni nzuri. Kwa hiyo hifadhi hii ya awali itasaidia mwaka 2014

FAO inasema kwa mwaka 2014 mazao yalitarajiwa kuleta unafuu kwa baadhi ya nchi kusini mwa Afrika kufuatia mavuno kidogo lakini ugawaji finyu wa mahindi na bei za juu za vyakula zinatarajiwa kuendelea katika maeneo yeneye idadi kubwa ya watu.