Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asilimia tano ya watu duniani wana matatizo ya uziwi: WHO

Asilimia tano ya watu duniani wana matatizo ya uziwi: WHO

Tukiwa tunaelekea siku ya kujali masikio duniani hapo March 3, Shirika la Afya duniani WHO linakadiria kuwa zaidi ya asilimia tano ya watu duniani ambayo ni sawa na watu milioni 360 wana tatizo la uziwi. Taarifa zaidi na Flora Nducha

(TAARIFA YA FLORA)

Kwa mujibu wa taarifa ya WHO idadi kubwa ya watu hao wako Asia Pasific, Asia ya Kusini na ukanda wa kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika. WHO inasema nusu ya visa vya kusikia duniani huzuilika na kutibika kirahisi. Kadhalika shirika hilo la afya ulimwenguni linasema ni nchi 32 kati ya 76 ambazo zimechukua hatua kufuati autafiti huo wa WHO na kuanzisha mikakati ya kuzuia magonjwa na uziwi.

Kwa mujibu wa shirika hilo nchi nyingi zina upungufu wa wataalamu, vifaa vya kutoa elimu na mifumo ya data pamoja na mipango ya kuwahudumia wenye ulemavu wa kusikia.

Shelly Chadha ni dk kutoka WHO

(SAUTI DK SHELLY)