Uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga ubaguzi wa aina yoyote wafanyika leo

27 Februari 2014

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloongoza mapambano dhidi ya Ukimwi, UNAIDS Michel Sidibé ameshiriki uzinduzi wa harakati za kuelekea kilele cha siku ya kimataifa ya kupinga aina zote za ubaguzi Machi Mosi.

Siku hii inalenga kutoa wito kwa watu popote pale walipo kuendeleza na kutambua haki ya kila mmoja kuishi maisha yenye utu bila kujali muonekano, jinsi, ampendaye na hata uwezo wake wa kiuchumi. Nembo ya siku ya kutokomeza aina zote za ubaguzi duniani ni kipepeo kinachotambuliwa kwa uwezo wake wa kubadilika.

Miongoni mwa wanaosongesha kampeni hiyo ni mwanamuziki mashuhuri kutoka Mali Toumani Diabaté ambaye ni balozi mwema wa UNAIDS.

(Sauti ya Diabate)

Naamini katika ulimwengu usio na ubaguzi wowote! Funguka na shiriki!onyesha mshikamano wako kwa kutumia nembo ya kipepeo! Pamoja tutatokomeza ubaguzi wa aina zote.”

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter