Hali ya huduma kwa watu walio taabani kutokana na maradhi ina katisha tamaa

Hali ya huduma kwa watu walio taabani kutokana na maradhi ina katisha tamaa

Ripoti mpya iliyotolewa hivi karibuni kuhusu huduma kwa watu walio taabani kutokana na maradhi imeonyesha kuwa hali ya huduma hiyo ni mbaya zaidi kwenye nchi zinazoendelea. Mathalani inasema kuwa wagonjwa walio taabani kutokana na magonjwa kama vile saratani, moyo, kisukari na hata kiharusi hupata machungu ya maumivu bila tiba huku uangalizi ukiwa wa taabu.  Takwimu zinasema ni mtu mmoja kati ya 10 ndiye anayepata huduma ya tiba ya kupunguza maumivu ya magonjwa anapokuwa taabani na kukaribia kupoteza maisha.

Waandaaji wa ripoti hiyo ni shirika la afya duniani, WHO kwa kushirikiana na kikundi cha ushirikiano wa huduma za kupunguza machungu ya magonjwa mtu awapo taabani, WPCA.