Tulinde tamaduni nzuri zile potofu tuachane nazo: Ban

6 Februari 2014

Tunapaswa kulinda mazuri yote kwenye tamaduni zetu na kuachana na zile ambazo zinatuathiri, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kwenye ujumbe wake wa siku ya kutokomeza ukeketaji kwa wanawake na watoto wa kike hii leo.

Amesema hakuna sababu yote iwe ya kiafya, kimaendeleo au kidini ya kuendeleza mila hiyo potofu na kwa kuwa eti imekuwepo muda mrefu siyo msingi wa kuihalalisha.

Yakadiriwa kila mwaka wasichana Milioni Tatu wenye umri wa miaka 15 hukeketwa ambapo nchini Tanzania Mtaalamu wa masuala ya jinsia kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA Christine Kwayu jitihada zimefanyika kuondokana na mila hiyo potofu.

(Sauti ya Christine)

Katika ujumbe wake mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu wa UNFPA amezitaja Kenya, Uganda, na Guinea-Bissau kuwa nchi tatu za Afrika zilizopitisha sheria za kuharamisha kitendo hicho.