Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yaonya kuhusu tishio la njaa Sudan Kusin

FAO yaonya kuhusu tishio la njaa Sudan Kusin

Shirika la chakula na kilimo duniani,  FAO limeonya juu ya uwezekano wa kujitokeza kwa hali mbaya ya ukosefu wa chakula huko Sudan Kusini ambako kiasi cha watu milioni 3.7 wako katika hali ngumu wakihitaji misaada mbalimbali ikiwemo chakula. Taarifa kamili na George Njogopa.

(George Njogopa)

FAO imetoa mwito ikihitaji kiasi cha dola za Marekani milioni 77 ili kukwamua hali ngumu inayoliandama taifa hilo lililotumbukia kwenye mapigano ya kikabili tangu mwaka uliopita baada ya wakubwa wa kisiasa kuhasimiana.

Machafuko hayo yamesababisha pia kupanda kwa bidhaa za chakuka huku nyingine zikiadimika kabisa jambo ambalo limezidi kuwatia wasiwasi wananchi wa eneo hilo.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na wahisani wake yameanzisha juhudi za kukabiliana na hali jumla ya mambo na sasa inahitaji kiasi cha dola za Marekani milioni 1.27 ili kufikia shabaha yake ya utoaji misaada ya usamaria mwema.

Inakadiria kwamba zaidi ya  watu milioni 7 wapo hatarini kukubwa na kitisho cha ukosefu wa chakula katika taifa hilo jipya ulimwenguni .Watu wengine 870,000 wamelazimika kuyakimbia makazi yao na kwenda uhamisho ikiwa ni jaribio la kunusuru maisha yao kutokana na machafuko yanayoendelea.