UM na wadau watoa ombi jipya kusaidia wenye njaa barani Afrika

3 Februari 2014

Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na wahisani wake leo imezindua mpango ambao umelenga kutoa msaada kwa mamilioni ya watu barani Afrika. Mpango huo wa miaka mitatu una shabaha ya kukusanya kiasi cha dola za Marekani bilioni 2 kutoka kwa wafadhili mbalimbali. Taarifa zaidi na George Njogopa

(Ripoti ya George Njogopa )

Kulingana na takwimu zilizopo, kiasi cha watu zaidi ya milioni 20 wapo hatarini kukubwa na janga la njaa katika eneo la Sahel na baadhiyao wanahitaji msaada wa haraka.

Pia inakadiriwa kwamba zaidi ya watoto milioni 5 waliochini ya umri wa miaka mitano wanaweza kutumbukia katika janga la kukubwa na tatizo la utapiamlo katika kipindi cha mwaka 2014.

Hali ya mapigano pamoja na kukosekana kwa usalama kumewalazimu zaidi ya watu milioni 1.2 kuyakimbia makaziyaona kwenda kuishi uhamishoni kwa hofu ya usalama wamalizao.

Mpango huo uliozinduliwa leo umezilenga kuzipiga jeki nchi zaBurkina Faso,Cameroon,Chad,Gambia,MalinaMauritania. Nyingine ni Senegal,NigernaNigeria.

Akizungumza mjini Roma, Mratibu wa mpango huo Valerie Amos amesema  kuwa idadi ya watu wanaohitaji msaada wa dharura imeendelea kuongezeka na kwamba kadri hali inavyozidi kuwa mbaya ndivyo inavyobomoa ustawi wa wananchi wa eneohilo.

FAO ni moja ya wabia wa mpango huo wa usaidiziSahelna Rodrigue Vinet ni Mratiibu mkuu katika kitengo cha Maswala ya dharura na marekebisho …

Mpango huo una nia tatu kwanza ni kuwafikishhia msaada wale ambao wanahitaji ili waweze kupanda na kuzalisha cahkula chao na kama itawezaekana kuimarisha mazao ili wawe na chakula cha kutosha mwaka ujao. Jambo la pili ni kuimarisha mfumo wa dhalili za mapema ili kuhakikisha kwamba na habari ya kile kinachoendelea ili tuweze kutabiiri na kukabiliana na mzozo kabla ya athari. La tatu ni kupunguza gharama 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter