Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua mwakilishi mpya wa UNSMIL:Ould Cheikh Ahmed

Ban amteua mwakilishi mpya wa UNSMIL:Ould Cheikh Ahmed

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua Ismail Ould Cheikh Ahmed wa Mauritania kama Kaimu mwakilishi Maalum na Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL ambako pia atashikilia nafasi ya Mratibu mkazi wa Mpango wa Umoja huo.

Bwana Ould Cheikh Ahmed anachukua nafasi ya Georg Charpentier wa Finland ambaye ameshikilia nafasi hiyo tangu Oktoba 2011. Katibu Mkuu amemshukuru Charpentier kwa kujitoa kwake wakati akishikilia nyadfa hiyo na kwa ,mchango wake kwa UM nchini humo.

Bwana Ahmed ana uzoefu wa miaka 27 ndani ya Umoja wa Mataifa katika maswala maendeleo na utoaji wa misaada ya kibindamu barani Africa, Mashariki ya kati na Ulaya masjhariki. Amewahi kuwa mwakilishi Mratibu mkazi nchini Syria kati ya mwaka 2008-2012 na Yemen kati ya mwaka 2012-2014.

Pia ameshikilia nafasi tofauti katika shirika la kuhudumia watoto UNICEF ikiwemo kama Mkurugenzi msimamizi maswala ya mabadiliko mjini New York, kaimu Mkurugenzi wa Afrika mashariki na Kusini, Nairobi na mwakilishi Georgia.

Bwana Ould Cheikh Ahmed ana shahada ya juu kuhusu maswala ya Raslimali ya maendeleo kutoka chuo cha Manchester Uingereza na shahada ya uchumi kutoka chuo kikuu cha Montpellier Ufaransa. Bwana Ould Cheikh Ahmed aliyezaliwa mwaka 1960 na ana ujuzi wa lugha ya Kingereza, kifaransa na kiarabu.