Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi Sudan Kusini watoa ushirikiano kulinda mustakhbali wao: UNHCR

Wakimbizi Sudan Kusini watoa ushirikiano kulinda mustakhbali wao: UNHCR

Wakimbizi wa ndani huko Sudan Kusini wamejikuta wakilazimika kusaidiana na wafanyakazi wa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR ili kuziba pengo la watendaji na kuhakikisha majukumu ya kuwapatia usaidizi yanafanyika bila kikwazo chochote. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Ripoti ya Assumpta)

Mkuu wa operesheni za shirika hilo kwenye eneo la Bunj jimbo la Upper Nile, Adan Ilmi amesema idadi ya maafisa inayotakiwa ni 85 lakini waliopo ni 18, hivyo wakimbizi wanatoa msaada kwenye majukumu kama vile ulinzi wa bohari. Amesema bohari hizo za UNHCR na mashirika mengineyo yaliyokimbia kutokana na ghasia, zina vifaa vya usaidizi na hivyo wakimbizi wanaimarisha ulinzi kuhakikisha hakuna uporaji.

 Amesema wakati wakimbizi wanafanya jukumu hilo, maafisa wa UNHCR wanafanya kazi kama vile ujenzi wa miundombinu iliyoharibika. Mwakilishi wa UNHCR nchini Sudan Kusini Cosmas Chanda amesema ni jambo la busara kuwa wakimbizi wamebeba kwa hiari jukumu hilo na wanatambua mchango wao.