Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban awateua Kufour na Stolternberg kumsaidia masuala ya mabadiliko ya tabianchi

Ban awateua Kufour na Stolternberg kumsaidia masuala ya mabadiliko ya tabianchi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametangaza kuwateuwa wajumbe wawili ambao watawajibika katika eneo la mabadiliko ya tabia nchi. Walioteuliwa ni rais mstaafu wa Ghana John Kufuor na waziri mkuu wa zamani wa Norway Jens Stoltenberg. Ban amewataka wajumbe hao kuzunguka duniani kote na kuwa na majadiliano na viongozi wa kiserikali ili kuongeza utashi wa kisiasa kabla ya kufanyika kwa mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabi nchi hapo mwakani 2014. Mkutano huo ambao utatoa mtazamo mpya kuhusiana na suala la mabadiliko ya tabia nchi umepangwa kufanyika Septemba 23, mjini New York.