Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mandela alitetea maadili ya haki na maridhiano: Rais Baraza la usalama

Mandela alitetea maadili ya haki na maridhiano: Rais Baraza la usalama

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo walilazimika kusitisha kikao chao cha kupokea ripoti kuhusu mahakama za za uhalifu wa kimbariRwanda, ICTR na mahakama ya uhalifu ya taifa la zamani laYugoslavia, ICTY ili kuugana na ulimwengu kwenye maombolezo ya kifo cha Mzee Nelson Mandela.

Wajumbe walisimama kwa dakika moja kumkumbuka Mzee na Mandela na kufuatia na kauli kutoka kwa Rais wa barazahiloBalozi Gerard Araud kutoka Ufaransa akasema..

(Sauti ya Balozi Gerard)

 Kwa niaba ya baraza la usalama naamini kuwa tunaweza kusema kwamba tunaungana na hisia na uchungu baada ya kusikia taarifa hizi. Na Umoja wetu unaendana na maadili ambayo Mzee Mandela alikuwa anatetea. Maadili ya haki na maridhiano. Vyote vinaenda pamoja.”