Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Kimataifa ya Mandela

Siku ya Kimataifa ya Mandela

Leo ni Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela, shujaa wa kupigania uhuru Afrika Kusini na mpiganiaji haki za binadamu, ambaye leo ikiwa siku ya kuzaliwa kwake, amehitimisha miaka 95.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeadhimisha siku hii kwa kuangalia video fupi ya Mandela, akiongea nyakati tofauti, ukiwemo mwaka 1990, alipotoa hotuba kwenye Umoja wa Mataifa

CLIP MANDELA

“Daima litabaki doa lisilofutika katika historia ya mwanadamu kuwa uhalifu wa ubaguzi wa rangi uliwahi kuwepo. Daima litabaki shtaka kwa wake na waume wote wenye busara, ya kwamba ilituchukuwa muda huu mrefu, kabla ya sote kusimama na kusema, uhalifu huu hauwezi kukubalika tena.”

Kumekuwepo pia hotuba za kumuenzi Mandela, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, amesema Nelson Mandela ni shujaa na gwiji wa nyakati zetu

“Alitoa miaka 67 ya maisha yake kwa kupigania haki za binadamu. Kwenye siku hii ya Kimataifa, Umoja wa Mataifa na Wakf wa Mandela zinatoa wito kwa watu kote duniani kutoa angaa dakika 67 kwa huduma ya jamii. Leo, na kila siku tunataka kuchagiza familia ya ubinadamu kuchukuwa hatua, kuchagiza mabadiliko, na kujenga ulimwengu endelevu, wenye amani, na usawa.”

 

Miongoni mwa watu mashuhuri ambao wametoa hotuba ni rais mstaafu wa Marekani Bill Clinton,

CLINTON

Kwenye Baraza Kuu pia amezungumza Mzee Andrew Mlangeni, mwenye umri wa miaka 87, ambaye alifungwa Nelson Mandela kwenye kisiwa cha Robben na angali rafikiye wa karibu,