Mandela Akumbukwa

Baraza Kuu lamkumbuka Nelson Mandela

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo limefanya kikao maalumu cha kumkumbuka Hayati Nelson Mandela, siku chache baada ya kuzikwa kwake siku ya Jumapili. Joshua Mmali na taarifa kamili

(TAARIFA YA JOSHUA)

Sauti -

Baraza Kuu lamkumbuka Nelson Mandela

WFP imetoa wito wa kumuenzi Nelson Mandela kwa kutokomeza njaa:

Mkuu wa shirika la mpango wa chakula duniani (WFP) Ertharin Cousin Alhamisi ametoa wito wa kumuenzi hayati Nelson Mandela kwa kutokomeza njaa katika watu wetu.

Sauti -

WFP imetoa wito wa kumuenzi Nelson Mandela kwa kutokomeza njaa:

Wakati Mandela akipumzika kwa amani ni wakati wa kumuenzi kwa vitendo:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ameungana na mamilioni ya watu wa Afrika ya Kusini, familia ya Marehemu Nelson Mandela, viongozi mbalimbali , watu mashuhuri na dunia kwa ujumla kutoa heshimazake za mwisho kwa jabali la Afrika na mtetezi wa haki duniani mzee Madiba, Nelson Mandela.

Sauti -

Wakati Mandela akipumzika kwa amani ni wakati wa kumuenzi kwa vitendo:Ban

Ban amsifu Mandela kama jabali wa haki na usawa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, ambaye yuko Afrika Kusini, amemsifu tena Hayati Mzee Nelson Mandela kama mtu aliyekuwa jabali wa haki, usawa na haki za binadamu.

Sauti -

Ban amsifu Mandela kama jabali wa haki na usawa

Kosa lililomfanya Mandela afungwe ni kupigania Haki:Mbotela

Mzee Mandela ni kiongozi ambaye anatambulika kote ulimwenguni, umaarufu wake atakumbukwa na wengi hususani wale waliomshuhudia. Miongoni mwao ni mwandishi mashuhuri Afrika Mashriki Leornard Mambo mbotela kutoka Kenya.

Sauti -