Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mipango kukabiliana na athari zisizoepukika za mabadiliko ya hali ya hewa inafanywa:UNFCCC

Mipango kukabiliana na athari zisizoepukika za mabadiliko ya hali ya hewa inafanywa:UNFCCC

Wakati wawakilishi kutoka nchi mbalimbali wanakutana Warsaw, Poland kwenye mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa, nchi masikini kabisa duniani zinakamilisha mipango ya kukabiliana na athari zisizoepukika za mabadiliko ya hali ya hewa .

Mikakati hiyo inasaidiwa na mpango wa Umoja wa Mataifa wa mkataba wa mabadiliko ya hali ya hewa UNFCCC, kitengo cha kimataifa cha mazingira GEF na mashirika mengine ya Umoja wa mataifa. Kwa mujibu wa UNFCCC nchi zote 48 masikini ambazo ni sehemu ya UNFCCC kwa sasa zimewasilisha mipango yake ya kitaifa .

UNFCCC inasema kwa mipango hiyo inayokamilishwa nchi masikini zitaweza kutathimini vyema na mara moja athari za mabadiliko kama ukame na mafuriko na ni msaada gani wanaohitaji ili kukabili athari hizo. Imeongeza kuwa sayansi inaonyesha kwamba kiasi kikubwa cha mabadilo hakiepukiki mfano kimbunga cha wiki jana Ufilipino.